Msimu uliopita, Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki aliweka jina lake katika historia ya soka la Tanzania kwa kile alichoifanyia Yanga
Mfungaji bora, kiungo na mchezaji bora wa msimu ni tuzo alizoondoka nazo mwishoni mwa msimu
Haikuwa kazi rahisi kwa uongozi wa Yanga kumbakisha Aziz Ki ambaye alipokea ofa nyingi kutoka ndani na nje ya Afrika
Msimu huu bado haujawa mzuri kwake ukilinganisha na kile alichofanya msimu uliopita
Wale wasimtakia mema wamepata mwanya wa kumshambulia kwa kila aina ya maneno wengine wakifika mbali zaidi kuingia maisha yake binafsi nje ya soka
Wasichofahamu ni kuwa kila mchezaji hupita katika nyakati ngumu. Wazungu wana msemo wao unaosema 'form is temporary but class is permanent' ikimaanisha mchezaji bora anaweza kupita katika vipindi vifupi vya changamoto ambavyo huisha
Katika msimu huu Aziz Ki amehusika katika mabao manne, akifunga moja ya kutoa pasi tatu za mabao
Sio takwimu nzuri kwa kulinganisha na kile alichofanya msimu uliopita baada ya mechi 10 lakini sio takwimu mbaya kwa kuzingatia ushindani uliopo msimu huu
Feisal Salum na Jean Ahoua ndio wachezaji pekee waliomzidi Aziz Ki idadi ya pasi za mabao wakiwa nazo nne huku yeye akiwa na tatu
Mapema kabla ya msimu kuanza Aziz Ki aliweka wazi hana mpango wa kuwania tuzo ya ufungaji bora kwa kuwa sasa Yanga ina washambuliaji bora ambao anaamini watafanya kazi ya kufunga huku yeye akijikita katika kutengeneza nafasi. Imekuwa bahati mbaya pia washambuliaji hawajawa na ufanisi uliotarajiwa
Wakati mwingine hizi kampeni za kumchafua Aziz Ki hufanywa kimkakati ili kuhakikisha hapati utulivu katika majukumu yake
Hao wanaofanya hivyo wanafahamu madhara Aziz Ki pale anapokuwa na utulivu wa kufanya kazi