Yanga leo imepoteza mchezo wa pili mfululizo ligi kuu ya NBC ikifungwa mabao 3-1 dhidi ya Tabora United katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex
Yanga haikuwa na mechi bora unaweza kusema kukosekana kwa mabeki Ibrahim Bacca, Dickson Job, Yao Kouassi na Chadrack Boka athari yake imeonekana leo
Kocha Miguel Gamondi alianza na beki mmoja tu wa asili Bakari Mwamnyeto na Aziz Andambwile ambaye hata hivyo alipata majeraha ndani ya dakika 10 za kwanza na hivyo Khalid Aucho kulazimika kucheza eneo la safu ya ulinzi
Pamoja na mapungufu hayo itoshe kusema Yanga haikucheza vizuri, kwani licha ya kumiliki mchezo haikutengeneza nafasi nyingi za wazi
Gamondi amewapongeza Tabora United kwa ushindi waliopata huku akibeba lawama ya kipigo hicho
ADVERTISE HERE