Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amewaambia wachezaji wa timu hiyo kuwa anataka kuona wanafanya kazi moja tu ya kusaka ushindi katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizobakia.
Kwenye kikao alichofanya juzi na wachezaji pamoja na benchi la ufundi, Zahera aliwaeleza maneno hayo wachezaji
Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema Zahera amesisitiza umuhimu wa kujituma kwa kila mchezaji kuhakikisha wanashinda kila mechi iliyoko mbele yao kwa sababu anaamini uwezo wa kupambana wanao.
"Kocha amewaambia wachezaji, hapa kazi, kazi," alisema kwa kifupi meneja huyo
Aliongeza kuwa kikosi hicho cha Yanga kinatarajia kurejea jijini leo kikiwa na ari, morali na nia ya kuondoka na pointi tatu.
"Ni mechi ngumu kama nyingine tulizowahi kucheza, lakini hii ni muhimu zaidi msimu huu kwa sababu itatoa sura ya mbio za ubingwa zinavyoelekea, tayari tuko nyuma ingawa tuna mechi mbili mkononi"
Aliongeza kuwa kocha huyo mpya amewataka wachezaji kusahau matokeo ya mechi zilizotangulia na kuongeza umakini katika mechi hiyo iliyo mbele yao kwa sababu kila mchezo unatumia dakika 90 na mbinu tofauti

ADVERTISE HERE