Kiungo wa Yanga Khalid Aucho amewashukuru mashabiki wa timu hiyo waliojitokeza kwa wingi uwanja wa Azam Complex katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc
Licha ya Yanga kupoteza mchezo huo, Aucho amewataka mashabiki waendelee kuiunga mkono timu yao kwani anaamini watarejea wakiwa imara zaidi
"Shukrani kwa mashabiki wetu kwa sapoti kubwa jana, huwa tunajipanga vyema ila Mwenyezi Mungu hupanga vyema zaidi"
"Naipongeza Azam Fc kwa ushindi wa jana na najua tutarudi tukiwa na nguvu kuliko wakati mwingine wowote"
"Tutaendelea kuipigania klabu hii pasipo kujali matokeo, tuonane tena baadae wananchi," aliandika Aucho katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Mchezo unaofuata kwa Yanga ni dhidi ya Tabora United utakaopigwa Novemba 07 katika uwanja wa Azam Complex