Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema wamekubali kupoteza mchezo dhidi ya Azam Fc, wanakwenda kujipanga ili wafanye vizuri kwenye mechi zinazofuata
Jana Yanga ilipoteza mechi ya kwanza msimu huu kwa kufungwa bao 1-0 na Azam Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex
Akizungumza baada ya mchezo huo, Gamondi alisema kama timu ya mpira wa miguu walifahamu kuna siku watapoteza mchezo
"Sikufurahishwa na matokeo lakini nawapongeza wachezaji wangu wameonyesha ujasiri mkubwa katika mchezo huu"
"Tulianza vyema mchezo lakini mambo yalibadilika baada ya kadi nyekundu. Nililazimika kubadili mfumo na tulitawala mchezo katika kipindi cha pili tukitengeneza nafasi mbili za wazi ambazo tulishindwa kuzitumia"
"Sitaki kulaumu wamuzi lakini kuna matukio yanashangaza. Tulipocheza na Simba Dube alifanyiwa madhambi na mchezaji wa Simba katika mazingira ambayo yanafanana kabisa na tuko lililomtokea Bacca leo. Imetolewa kadi nyekundu lakini mechi dhidi ya Simba haikutolewa"
"Nilizungumza na mwamuzi baada ya mchezo kiungwana kuhoji aina hii ya maamuzi lakini hatusemi hiyo ni sababu ya sisi kupoteza mchezo"
"Mara kadhaa nimezungumza na wachezaji wangu nikiwakumbusha ipo siku tutatopeza mchezo bila ya kujali tuko bora kiasi gani"
"Tunawapongeza Azam Fc kwa ushindi waliopate leo (jana), lazima tuheshimu matokeo ya mpira wa miguu," alisema Gamondi