Yanga imepoteza mchezo wa kwanza msimu huu ikikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex
Bao lililofungwa Gibril Sillar lilitosha kuihakikishia Azam Fc ushindi dhidi ya Yanga ambao ilimaliza ikiwa na wachezaji 10 uwanjani baada ya Ibrahim Bacca kutolewa nje kwa kadi nyekundu
Yanga ilicheza kwa takribani dakika 70 ikiwa pungufu lakini ilitawala mchezo huo kwa muda mwingi
Hata hivyo haikuwa rahisi kuipenya ngome ya Azam Fc ambao wote walirudi nyuma baada ya kufunga bao
Wachezaji wa Yanga walipambana kusaka angalau bao la kusawazisha licha ya mazingira magumu ya mchezo huo ambapo wananchi wamecheza mechi mfululizo huku wapinzani wao wakipata siku 9 za kujiandaa na mchezo huo
Alama tatu zimedondoka lakini bado Wananchi wako juu ya msimamo wa ligi