Gamondi afunguka maandalizi mchezo dhidi ya Azam Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Nov 2024
Gamondi afunguka maandalizi mchezo dhidi ya Azam Fc

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Azam Complex

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Gamondi amesema hautakuwa mchezo mwepesi kwao hasa ikizingatiwa wamepita katika kipindi cha ratiba ngumu ya kucheza mechi mfululizo

"Hatuna muda wa kutosha wa kujiandaa na mchezo, lakini tupo tayari kushindana na Azam FC. Utakuwa ni mchezo wenye msisimko wa aina yake kwangu na kwa kocha wa Azam kwani namfahamiana nae kwa miaka 25, utakuwa wasaa mzuri kati yetu"

"Kwenye maisha hupaswi kujiwekea matarajio asilimia mia moja, lolote linaweza kutokea, hiyo ndio tabia ya mpira wa miguu. Tunaweza kukosa wachezaji wengi. Nafahamu Azam wamepata zaidi ya siku saba mpaka nane za kujiandaa. Tumeshacheza michezo miwili wakati wao wakiwa wamepumzika. Lakini nashukuru nimebarikiwa kuwa na wachezaji wazuri sana"

"Naheshimu kila timu, Azam wana timu nzuri, wana kocha mzuri. Tutajitahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha tunapata alama tatu muhimu. Ni matarajio yangu tutacheza mchezo mzuri kuliko michezo iliyopita"

"Kila mchezo ni tofauti, na kila mpinzani ni tofauti. Kuna muda itabidi tubadilishe mfumo na tutafute njia na mfumo sahihi wa kupata matokeo dhidi ya Azam," alisema Gamondi

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, mlinda lango Aboutwalib Mshery amesema wachezaji wako tayari kwa mchezo huo na dhamira yao ni kuendeleza mwenendo wa ushindi

"Kwa sisi wachezaji maandalizi ni yale yale, wachezaji tunajua nini chakufanya isipokuwa mwalimu ndiye mwenye mipango bora zaidi, najua muda wa kujiandaa ni mchache lakini tupo imara na tumejiandaa vyema"

"Kazi yetu kama timu ni kuhakikisha kuwa tunapata alama tatu muhimu pamoja na cleansheets. Lengo kuu hasa ni kuendelea kusalia kileleni. Tuna timu bora kwenye kila eneo hivyo tunayo matumaini makubwa. Tunajiamini na tunaenda kushindana na timu mpya kwa sababu wana kocha mpya hivyo hatutaanglia ya nyuma," alisema

Yanga SC Stories

Yanga Princess bado haijajipata
Yanga Princess bado haijajipata
4m ago
READ MORE β†’
Pacome sasa anatembea bila magongo
Pacome sasa anatembea bila magongo
3h ago
READ MORE β†’
Manqoba katika maandalizi ya dabi ya pili
Manqoba katika maandalizi ya dabi ya pili
6h ago
READ MORE β†’
Mzize anaitaka dabi Oktoba 10
Mzize anaitaka dabi Oktoba 10
9h ago
READ MORE β†’
Kangwanda anauwasha moto Zambia
Kangwanda anauwasha moto Zambia
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 30 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 30 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya Kariakoo Derby
Maandalizi ya Kariakoo Derby
1d ago
READ MORE β†’
Edna Lema apania kumaliza uteja dhidi ya Simba Queens
Edna Lema apania kumaliza uteja dhidi ya Simba Queens
1d ago
READ MORE β†’
Familia ya Mzee Mpili yatoa shukrani kwa uongozi Yanga
Familia ya Mzee Mpili yatoa shukrani kwa uongozi Yanga
1d ago
READ MORE β†’
Zokouane, Shalulile uso kwa uso kufuzu Afcon 2027 leo
Zokouane, Shalulile uso kwa uso kufuzu Afcon 2027 leo
1d ago
READ MORE β†’