Mudathir Yahya na Maxi Nzingeli msimu uliopita walijipambanua kwa aina yao ya uchezaj kocha Migue Gamondi akiwatumia karibu kila mechi
Maxi anafahamika kwa uwezo wake wa kuwa kila sehemu dimbani, msimu huu akiwa tayari amepachika mabao matatu kwenye ligi
Mudathir ni kiungo 'bax-2-box', atakaba kama 'mbwa mwitu' pale timu inapokuwa haina mpira lakini utamkuta katika 'box' la timu pinzani pale timu inaposhambulia
Lakini kuna huyu fundi Duke Abuya ambaye Yanga ilimnasa kutoka klabu ya Ihefu Fc (sasa Singida Black Stars)
Abuya nae anafanya vyema majukumu ambayo Mudathir na Maxi huyafanya lakini yeye ni mahiri zaidi katika umiliki wa mpira
Uwezo mkubwa wa kupiga pasi na anapoweka mpira katika himaya yake ni ngumu kuchukua
Abuya ni mchezaji mwingine kiraka ambaye Gamondi amekuwa akimtumia katika maeneo tofauti
Juzi katika mchezo dhidi ya Singida BS, Gamondi alimuanzisha Abuya eneo la Mudathir na alionyesha kiwango bora sana, kama sio lile bao alilofunga Pacome Zouzoua, pengine ni Abuya ambaye angeondoka na tuzo ya nyota wa mchezo