Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema wale wanaodhani Yanga ni timu ya kawaida wataiheshimu pale watakapokutana nayo
Jana Yanga iliichapa Singida Black Stars bao 1-0 na kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 24
Yanga imeweka rekodi ya kushinda mechi zote nane walizocheza msimu huu tena pasipo kuruhusu bao
Kabla ya mchezo huo kocha wa Singida BS Patrick Aussems alisikika akisema haihofii Yanga kwa kuwa anaiona ya kawaida kama ilivyo Pamba au KenGold
Kauli hiyo hiyo ilimkera Gamondi ambaye baada ya kugawa dozi, akamkumbusha Mbelgiji huyo kuwa amekutana na kina kirefu kuliko alivyodhani huku akimtaka aweke heshima siku nyingine
"Sisi ni Yanga kuna muda tunavunjiwa sana heshima huwezi kuja kucheza na sisi ukaja kutulinganisha na Pamba au timu zengine kuna muda inabidi kumuheshimu mpinzani"
"Nilitarajia hili kuwa mchezo utakuwa mgumu sana ila sisi tumetengeneza nafasi zaidi yao na wao walikuwa wanacheza mipira ya juu pekee"
"Nimefurahishwa na performans ya wachezaji wangu wamecheza vizuri sana siku ya leo," alisema Gamondi