Mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Azam Fc ambao utachezwa Jumamosi Novemba 02, umerudishwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Mchezo huo awali ulipangwa kuchezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kulingana na taarifa iliyotolewa n Bodi ya ligi, mabadiliko hayo yamesababishwa na ukarabati unaoendelea katika uwanja wa Benjamin Mkapa
"Yanga walipeleka maombi yao kwa wamiliki wa uwanja kucheza mechi dhidi ya Azam Fc katika uwanja wa Benjamin Mkapa"
"Hata hivyo maombi hayo yamekataliwa kwa sababu wakandarasi waendelea na maboresho katika uwanja huo wakiwa wanakimbizana na muda"
"Hivyo kwa sababu hakuna muda zaidi kwa mwenyeji kuomba kutumia uwanja mwingine, basi mchezo huo unarudi katika uwanja wao wa nyumbani ambao ni Azam Complex," alisema Almas Kasongo ambaye ni mtendaji wa Bodi ya Ligi