Gamondi anazitaka alama tatu dhidi ya Singida BS

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Oct 2024
Gamondi anazitaka alama tatu dhidi ya Singida BS

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kikosi chake kiko Zanzibar kwa kazi moja tu, kuhakikisha wanashinda mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Black Stars na kurejea Dar es salaam na alama tatu

Yanga iliwasili Zanzibar mapema leo tayari kwa mchezo huo utakaopigwa kesho Jumatano Oktoba 30 katika uwanja wa New Amaan Complex

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Gamondi aliwashukuru mashabiki wa Yanga kwa kuwaongezea hamasa kila wanapokwenda kucheza

Gamondi amesema katika siku 21 kikosi chake kimecheza mechi 7, sio ratiba rahisi kwao lakini wamepata sapoti kubwa ya mashabiki wao na kuwaongezea nguvu kila wanaposhuka uwanjani

"Kwanza nina furaha kurejea tena hapa Zanzibar, kila Yanga inapokwenda huwa inategemea Ushindi, tupo hapa kwaajili ya Kushinda ingawa tunatambua Singida wana Kikosi kizuri na wamepata muda mrefu wa Kujiandaa"

"Tumecheza michezo 7 ndani ya siku 21, sio jambo jepesi kabisa kujiandaa katika mazingira haya. Changamoto kubwa tunayokumbana nayo sio tu michezo mingi kwa wakati mfupi bali uchovu wa safari. Tumetokea Arusha, awali ya hapo wachezaji wangu wengi walikuwa nje ya mipaka ya Tanzania. Leo tupo hapa na baada ya kesho tunapaswa kurejea Dar"

"Jambo zuri kwetu ni hamasa kubwa ya mashabiki kwani kila mahali tunapoenda ni kama tupo nyumbani. Binafsi niwapongeze sana na kuwashukuru mashabiki wetu popote Tanzania ambao wamekuwa wakiuunga mkono klabu yao kila inapocheza kwenye maeneo yao. Kila tunapoenda ni full House. Wengine wanakuja kutupokea Airport. Hii inaleta hamasa kubwa sana," alisema Gamondi

Yanga itakamilisha maandalizi yake ya mwisho katika uwanja wa New Amaan Complex, usiku wa leo tayari kwa mtanange huo

Yanga SC Stories

Yanga Princess bado haijajipata
Yanga Princess bado haijajipata
3m ago
READ MORE β†’
Pacome sasa anatembea bila magongo
Pacome sasa anatembea bila magongo
3h ago
READ MORE β†’
Manqoba katika maandalizi ya dabi ya pili
Manqoba katika maandalizi ya dabi ya pili
6h ago
READ MORE β†’
Mzize anaitaka dabi Oktoba 10
Mzize anaitaka dabi Oktoba 10
9h ago
READ MORE β†’
Kangwanda anauwasha moto Zambia
Kangwanda anauwasha moto Zambia
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 30 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 30 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya Kariakoo Derby
Maandalizi ya Kariakoo Derby
1d ago
READ MORE β†’
Edna Lema apania kumaliza uteja dhidi ya Simba Queens
Edna Lema apania kumaliza uteja dhidi ya Simba Queens
1d ago
READ MORE β†’
Familia ya Mzee Mpili yatoa shukrani kwa uongozi Yanga
Familia ya Mzee Mpili yatoa shukrani kwa uongozi Yanga
1d ago
READ MORE β†’
Zokouane, Shalulile uso kwa uso kufuzu Afcon 2027 leo
Zokouane, Shalulile uso kwa uso kufuzu Afcon 2027 leo
1d ago
READ MORE β†’