Kikosi cha Yanga leo kinaelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Black Stars
Kesho Jumatano, Oktoba 30 Yanga itashuka katika uwanja wa New Amaan Complex kumenyana na Singida BS katika mchezo wa kuamua hatma ya nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi
Wiki hii Yanga inakabiliwa na mechi mbili muhimu ambazo kama Wananchi wataibuka na ushindi watajiweka katika nafas nzuri kwenye mbio za ubingwa mapema tu
Baada ya mchezo dhidi ya Singida BS, Wananchi watarejea Dar kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya Azam Fc utakaopigwa Jumamosi, Novemba 02
ADVERTISE HERE