Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema wanakwenda Zanzibar wakiwa na matumaini makubwa ya kushinda mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Black Stars utakaopigwa Jumatano, Oktoba 30 katika uwanja wa New Amaan Complex
Kamwe amesema Singida BS wamefanya makosa makubwa kupeleka mchezo huo Zanzibar kwani dimba la New Amaan Complex ni Ngome ya Yanga
"Tuna mafunzo mawili ya kuwapa Singida Black Stars. Kwanza ni kuwaonyesha kwa vitendo kuwa wamejichanganya kuipeleka mechi kwenye ngome yetu"
"Yanga ndio mfalme wenye Visiwa vya Zanzibar Tunakwenda kuhakikisha Uwanja wa Amaan unakuwa na rangi mbili tu, KIJANI NA NJANO"
"Lakini pia tutawaonyesha kuwa msimamo wa ligi kuu unapendeza pale Yanga anapokuwa kileleni," alitamba Kamwe
Kikosi cha Yanga knatarajiwa kuelekea Zanzibar leo Jumanne tayari kwa mchezo huo ambao kama Yanga itaibuka na ushindi, itapanda kileleni mwa msimamo wa ligi kwa mara ya kwanza msimu huu