Kwa sasa unaweza kusema mshambuliaji Prince Dube yuko katika presha kubwa akisaka bao lake la kwanza katika ligi kuu ya NBC msimu huu
Baada ya Jean Baleke kufunga katika mchezo dhidi ya Coastal Union juzi, ni Dube pekee ambaye bado hajazifumania nyavu miongoni mwa washambuliaji wa Yanga
Clement Mzize alipachika bao katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Kennedy Musonda akapachika katika mchezo dhidi ya Pamba Jiji na Baleke kuwafunga Coastal Union juzi
Dube alianza vyema msimu huu akifunga mabao manne katika mechi za hatua ya awali ligi ya mabingwa, bao moja akifunga katika michuano ya Ngao ya Jamii
Ni suala la muda tu, nae ataandikisha jina lake katika wafungaji ligi kuu kwani alichokosa katika mechi zilizopita ni bahati tu
Washambuliaji wote wa Yanga msimu huu hawajaanza vyema kwenye ligi, ukimuondoa Dube wengine wamepachika bao moja moja tu
Kinara wa mabao ni Maxi Nzengeli aliyefunga mabao matatu akifuatiwa na Ibrahim Bacca aliyefunga mabao mawili