Tukutane Sheikh Amri Abeid kutegua mtego

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Oct 2024
Tukutane Sheikh Amri Abeid kutegua mtego

Ukiiangalia ratiba ya Yanga kwa undani ni kama kuna 'mitego' wametegewa Wananchi ili angalau wadondoshe alama katika mechi zao zinazofuatana

Baada ya 'kuvuka salama' katika mechi ya Derby dhidi ya Simba ambayo ilikuwa 'mtego' kwa Wananchi waliokuwa na wachezaji wengi katika timu za Taifa, mchezo uliofuata dhidi ya JKT Tanzania nao Wananchi wakaruka kihunzi

Leo wako uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuikabili Coastal Union katika mchezo mwingine mgumu

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kuwaongezea wachezaji wao ari ya kupambana

Kamwe amesema kuna watu hawapendi kuona Yanga inashinda kila mechi lakini watahakikisha wanaendeleza vipigo

"Niwaambie mashabiki wetu mje kwa wingi uwanja wa Sheikh Amri Abeid, nafahamu kuna watu hawapendi hivi tunavyoshinda kila siku lakini kwa umoja wetu, hawatatuzuia"

"Kama tutaweza kushinda mechi zote zinazofuata katika ratiba yetu, basi tutasafisha njia yetu kuelekea ubingwa wa nne mfululizo mapema," alisema Kamwe

Baada ya mchezo dhidi ya Coastal Union leo, Yanga inapaswa kusafiri kuelekea visiwani Zanzibar kuikabili Singida BS Oktoba 30 katika uwanja wa New Amaan Complex

Siku tatu baadae Yanga inapaswa kurejea Dar es salaam kuchuana na Azam Fc Novemba 02

Kama sio upana wa kikosi cha Yanga, isingekuwa rahisi kucheza mechi hizi ngumu mfululizo lakini vijana wa kocha Miguel Gamondi watapambana na bila shaka 'watatoboa'

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
3h ago
READ MORE β†’
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mwenda aanza mazoezi Yanga
Mwenda aanza mazoezi Yanga
19h ago
READ MORE β†’
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
23h ago
READ MORE β†’
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
Highlights : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’