Jana Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) lilitangaza tuzo za Shirikisho hilo kwa waliofanya vizuri msimu uliopita 2023/24 zitatolewa huko Morocco Disemba 16
Kwa msimu wa pili mfululizo, Yanga imeingia katika kipengele cha klabu bora Afrika sambamba na watani zao Simba
Lakini pia mlinda lango Djigui Diarra akatajwa katika kipengele cha mlinda lango bora Afrika akiiwakilisha Yanga na timu ya Taifa ya Mali
Kocha Miguel Gamondi ambaye alifanya vizuri na kikosi cha Yanga msimu uliopita hayumo katika kinyan'ganyiro cha kocha bora
Katika msimu wake wa kwanza na Yanga, Gamondi aliwaongoza Wananchi kushinda mataji yote ya ndani (Ligi Kuu na FA) na kuipeleka Yanga robo fainali ya ligi ya mabingwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 25
Ikumbukwe kabla ya ujio wa Gamondi, Yanga haikuwa imecheza hata hatua ya makundi katika miaka 25 iliyopita
Hata Nasreddine Nabi ambaye msimu wa 2022/23 aliiongoza Yanga kucheza fainali ya CAF CC huku akishinda mataji yote ya ndani, jina lake halikuwemo katika kinyan'ganyiro cha kocha bora 2023
Lakini utashangaa mwaka huu kuona jina la kocha wa Al Hilal Florent Ibenge likiwa katika orodha ya hiyo licha ya kuwa timu yake haikufanya maajabu msimu uliopita
Hapa ndipo utakapogundua hizi tuzo wakati mwingine zinaandaliwa kwa ajili ya watu maaalum na wengine wanashirikishwa tu kukamilisha ratiba