Tuzo za mwaka za CAF 2024 zitaandaliwa katika jiji la kitalii la Marrakech, Morocco, tarehe 16 Desemba 2024, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetangaza
Hii ni mara ya tatu mfululizo Morocco kuandaa sherehe hizo, baada ya kuandaa kwa mafanikio makubwa katika miaka miwili iliyopita
Klabu ya Yanga imeingia katika kinyan'ganyiro kwa mwaka wa pili mfululizo ikitajwa katika kipengele cha klabu bora ya mwaka
Aidha mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra nae ameingia katika kinyang'anyiro kwa mara ya pili akiwania tuzo ya golikipa bora wa mwaka
ADVERTISE HERE