Jumamosi ya wiki hii mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga watakuwa ugenini dimba la Sheikh Amri Abeid kuikabili Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya NBC, raundi ya saba
Kikosi cha kocha Miguel Gamondi kitakuwa kikisaka ushindi wa saba mfululizo msimu huu na pengine kukaa juu ya msimamo wa ligi kwa mara ya kwanza iwapo Singida BS watakosa ushindi dhidi ya Fountain Gate hapo kesho
Yanga inatarajiwa kusafiri kuelekea mkoani Arusha baadae leo ambapo kesho Ijumaa, Wananchi watakuwa na nafasi ya kufanya mazoezi yao ya mwisho katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambao unatumiwa na Coastal Union
Yanga ndio timu pekee inayoshikilia rekodi ya kutoruhusu bao msimu huu, ikifunga mabao 11 katika mechi 6 zinazowafanya wakusanye alama 18
Wananchi wamepania kuendeleza rekodi hiyo mkoani Arusha Jumamosi