Viungo washambuliaji Clatous Chama na Pacome Zouzoua jana waliteka 'shoo' uwanja wa Azam Complex wakiisaidia Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Pacome alifunga bao la kwanza la Yanga dakika ya 23 akimalizia pasi kutoka kwa Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka' ambaye aliandikisha 'assist' yake ya kwanza msimu huu
Kwenye dakika ya 44, Chama akarudi tena kwenye 'headline' akifunga bao la pili kupitia mpira wa adhabu nje kidogo ya 18
Ni baada ya mlinda lango wa JKT Tanzania kudaka shuti la Pacome nje ya eneo lake na hivyo kupelekea mkwaju huo wa adhabu ambao ulienda sambasamba na kadi nyekundu
Baada ya mchezo huo kumalizika, Pacome alitajwa nyota wa mchezo. Chama na Pacome kila mmoja amefunga bao moja katika ligi kuu msimu huu na kutoa pasi moja ya bao
Unaweza kusema sasa nyota hao wameanza rasmi ligi msimu huu