Baada ya kuwaachia kilio na maumivu makali watani zao Simba, Yanga leo inarudi tena dimbani kucheza mechi nyingine ya ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania. Ni katika uwanja wa Azam Complex mchezo huo utapigwa saa 1 usiku
Yanga inakwenda katika mchezo huo ikiwa na dhamira moja tu, kusaka ushindi kuendeleza rekodi ya kushinda kila mechi msimu huu
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi leo anatarajiwa kufanya 'rotation' ya kikosi chake baadhi ya nyota ambao hawakutumika katika mchezo uliopita dhidi ya Simba huenda wakaanza leo
Kiungo Khalid Aucho hatakuwa sehemu ya mchezo huo akiwa na kadi tatu za njano
Msimu uliopita Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya JKT Tanzania katika dimba la Azam Complex
Gamondi amesema mchezo wa leo utakuwa tofauti, jambo muhimu kwa kikosi chake ni kuibuka na ushindi