Ni ubabe ubabe Yanga imeendeleza dhidi ya watani zao Simba leo ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Bao la dakika ya 86 Maxi Nzengeli akipiga shuti lililojazwa kimiani na Kelvin Kijiri akijifunga katika harakati za kuokoa mpira
Ulikuwa mpira wa faulo uliopigwa na Clatous Chama uliokolewa na mlinda lango wa Simba Moussa Camara Maxi akakutana nao na kupiga shuti lililopelekea bao hilo
Ulikuwa mchezo uliojaa matukio mengi, mwamuzi Ramadhani Kayoko akifanya makosa mengi ya kibinadamu ikiwemo kuwanyima Yanga mkwaju wa penati baada ya Musonda kufanyiwa madhambi na mlinda lango Camara katika eneo la hatari
Ni ushindi muhimu kwa Yanga unaowapandisha katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 15
Aidha ni ushindi wa nne mfululizo kwa Yanga dhidi ya Simba. Itoshe kusema Simba sasa ni wateja wa kudumu...!