Maxi Nzengeli alifunga bao pekee la ushindi dhidi ya Simba katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii uliopigwa August 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa. Leo tena Simba na Yanga zinakutana katika uwanja huo wakati huu ukiwa ni mchezo wa ligi kuu
Ni aina nyingine ya mechi ambayo itaamuliwa na mbinu za makocha na ubora wa mchezaji mmoja mmoja. Katika makaratasi, Yanga inapewa nafasi kubwa ya kushinda kwa sababu inaonekana kuwa na timu bora zaidi na ina wachezaji wengi ambao wanaweza kuamua mchezo huo
Mshambuliaji Prince Dube ameifunga Simba mabao mengi zaidi kuliko timu yoyote tangu alipotua nchini kuitumikia Azam Fc kabla ya kusajiliwa na Yanga msimu huu. Dube ni silaha muhimu kwa Yanga siku ya leo
Stephane Aziz Ki ni mchezaji mwingine mwenye rekodi ya aina yake dhidi ya Simba tangu akiwa na klabu ya Asec Mimosas, amefunga mabao matano, matatu akiyafunga akiwa na Yanga
Katika mechi zilizopita dhidi ya Simba, Aziz Ki alikuwa mchezaji muhimu katika kuhakikisha Yanga inafanya vizuri
Nzengeli pia yuko katika orodha hiyo ya wachezaji waliofunga mabao mengi dhidi ya Simba, akifunga mabao matatu katika msimu wake wa pili tangu atue Yanga. Pengine leo inaweza kuwa nafasi nyingine kwake kuendelea kupaleka kilio Msimbazi
Pacome Zouzoua licha ya kufunga bao moja kwenye dabi, amekuwa mchezaji hatari zaidi katika mechi alizocheza dhidi ya Simba
Pengine Pacome ndiye mchezaji anayewaumiza kichwa zaidi benchi la ufundi la Simba kwani sio jambo rahisi kumdhibiti
Katika mechi hii, Yanga pia ina silaha muhimu ambayo wameitoa kwa wapinzani wao, Clatous Chama
Chama tayari ameingia kwenye mfumo wa kocha Miguel Gamondi, leo waajiri wake hao wa zamani wajiandae kukabiliana nae
Ubora wa mlinda lango Djigui Diarra, safu ya ulinzi na kiungo ni sababu nyingine inayofanya mashabiki wa Yanga waingie uwanja wa Benjamin Mkapa leo wakiwa wanajiamini