Ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini hatimaye imewadia, ni mchezo wa Derby ya Kariakoo unaozikutanisha Simba na Yanga utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Kwa mara nyingine, mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga, wanashuka uwanjani kuwania alama tatu muhimu ili kuendeleza rekodi ya ushindi kwa asilimia 100 msimu huu
Ushindi dhidi ya Simba leo utaiweka Yanga kwenye nafasi nzuri katika mbio za ubingwa dhidi ya watani zao kwani Wananchi watahitaji kushinda mechi nyingine ya kiporo ili kuwa juu kwa tofauti ya alama tano
Licha ya kushinda mechi tatu zilizopita, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema historia haina nafasi katika kuamua matokeo ya mchezo wa leo
Gamondi alisema watacheza kwa kuiheshimu Simba, kwani anatambua ni timu kubwa yenye historia, wachezaji na benchi bora la ufundi. Lakini anahitaji kushinda mchezo huu ili kuendelea kujiweka nafasi nzuri katika msimamo wa ligi
Yanga inakwenda katika mchezo huu ikiwa na kikosi chake kamili, Farid Mussa ndio mchezaji pekee ambaye hatakuwa sehemu ya mchezo
Kila la kheri Wananchi...!