Kiungo wa Yanga Khalid Aucho amesema Watanzania wana kila sababu ya kumuunga mkono na kumtia moyo mshambuliaji kinda Clement Mzize
Akiwa mchezaji wa ndani, Aucho amesema Watanzania wanapaswa kujivunia uwezo kwani huenda siku za baadae akaipa heshima Tanzania katika medali ya soka kama ilivyokuwa kwa Mbwana samatta
"Mzize ni mchezaji mzuri, mnapaswa kumuunga mkono ili afike mbali", alisema Aucho katika mahojiano maalum na Yanga Media
"Huyu sio mgeni, ni mchezaji wenu, msipomuunga mkono ni nani atakuwa Samatta wa baadae?," alihoji Aucho
"Mzize anapata nafasi mbele ya wachezaji wakubwa Yanga kama Dube, Musonda na Baleke maana yake amejipambanua na uwezo wake ni mkubwa," alisema Aucho
Aucho tayari amerejea nchini akiendelea na mazoezi ya Yanga kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa