Walter afunguka maandalizi Kariakoo Dabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Oct 2024
Walter afunguka maandalizi Kariakoo Dabi

Kikosi cha Yanga kinaendelea na maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi, Oktoba 19 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Habari njema kwa Yanga ni kuwa nyota wote waliokuwa na majukumu ya timu za Taifa, wanakamilisha majukumu yao leo na kesho Jumatano wanatarajiwa kuripoti Avic Town kwa ajili ya maandalizi ya mwisho

Meneja wa Yanga Walter Harrison amesema wachezaji ambao hawakuwa na majukumu ya timu za Taifa wamekuwa na muda mzuri wa kujiandaa na mchezo huo huku akiamini wale walioko timu za Taifa nao wamepata program nzuri za mazoezi

"Maandalizi yanaendelea vizuri kwa sehemu ya kikosi ambacho kiko Dar es Salaam, kama mnavyojua tuna kundi kubwa la wachezaji ambao wapo kwenye vikosi vya timu ya taifa, ila tunaamini kuwa wapo kwenye mikono salama na wanaendelea na maandalizi kuelekea kwenye michezo yao"

"Tunategemea wote watakuwa wamefika kambini Oktoba 16, kuelekea katika mchezo huo mkubwa na tarehe 17 na 18, siku hizo mbili tunazitumia kuwaweka vizuri kimwili na kiakili kwa ajili ya mchezo huo," alisema Harrison

Harrison amekiri changamoto ya ratiba kutokana na ukaribu wa mechi hiyo baada ya mechi za Kimataifa lakini matarajio yao ni kuwa wachezaji wote watarejea wakiwa salama kuweza kushiriki mchezo huo kikamilifu

"Ukiangalia ratiba ilivyo, na hawa wachezaji walio kwenye vikosi vya timu za taifa, hujui watarejea kwenye hali gani kiafya na kimwili, hivyo huwezi kutegemea nini kitatokea, lakini sisi tunaamini watarejea salama na tutakuwa kwenye wakati mzuri wa kukiandaa kikosi kuelekea kwenye mchezo huo muhimu kwetu kwani tunataka kuendeleza ushindi ili kuweza kuupata ubingwa mara ya nne mfululizo," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
8h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
12h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
13h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
13h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’