Stephane Aziz Ki na Burkina Faso jana walikuwa timu ya kwanza kujihakikishia tiketi ya kushiriki michuano ya Afcon 2025 baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burundi
Burkina Faso imefikisha alama 10 ikiungana na Senegal iliyopata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Malawi na kujihakikishia tiketi ya kushiriki michuano hiyo itakayofanyika Morocco
Aziz Ki amekamilisha majukumu yake ya timu ya Taifa na alitarajiwa kuondoka Ivory Coast baada ya mchezo huo kurejea Tanzania kuungana na wachezaji wengine wa Yanga wanaondelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaopigwa Oktoba 19
Nyota wengine wa Yanga ambao leo watakamilisha majukumu ya timu za Taifa ni Duke Abuya ambapo Kenya iko nyumbani kuumana na Cameroon
Prince Dube akiwa na Zimbabwe nae yuko nyumbani kumenyana na Namibia leo huku Khalid Aucho akitarajiwa kuiongoza Uganda katika mchezo wa ugenini dhidi ya Sudan Kusini kesho Jumanne
Kennedy Musonda na Zambia wako ugenini huko Chad kama ilivyo kwa Djigui Diarra na Mali ugenini dhidi ya Guinea Bissau
Ibrahim Bacca, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Mudathir Yahya na Clement Mzize wao watakuwa nyumbani hapo kesho na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' katika mchezo dhidi ya DR congo ambao utapigwa saa 10 jioni katika uwanja wa Benjamin Mkapa