Uongozi wa Yanga umemalizana na aliyekuwa kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya DR Congo, Mwinyi Zahera na sasa ndiye anayechukua mikoba ya George Lwandamina.
Kocha huyo aliyewasili nchini usiku wa kuamkia jana amekuwa kwenye mazungumzo ya siri na uongozi wa Yanga ambayo sasa yamefikia tamati kwa kocha huyo kutambulishwa.
Zahera Mcongo mwenye uraia wa Ufaransa alikuja na kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo ilivyokuja kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Tanzania mwishoni mwa mwezi uliopita.
Amekuwa kocha Msaidizi wa DR Congo kwa vipindi viwili tofauti mara ya kwanza akitumikia majukumu hayo mwaka 2015.
Zahera anayependa mfumo wa kujilinda na kushambulia kwa pamoja 'total football', amewahi kuvinoa vilabu kadhaa kama DC Motema Pembe na AFC Tubize.

ADVERTISE HERE