Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi kuu ya Vodacom Boniface Wambura amethibitisha Bodi hiyo kupokea malalamiko Yanga dhidi ya klabu ya Mbeya City.
Wambura amesema rufaa ya Yanga imewasilishwa kwa Kamati ya Saa 72 ambayo inasubiri ripoti ya mwamuzi na kamishna wa mchezo huo.
Γ’β¬ΕTumepata malalamiko ya Yanga kwa hiyo tunapeleka kwenye kamati inayohusika kwa ajili ya maamuzi na kikanuni tunasubiri ripoti ya mwamuzi na kamishna ambazo tunatakiwa tuzipate ndani ya saa 48Γ’β¬Β amesema Wambura
Kimsingi Yanga imewasilisha malalamiko matatu kwa Bodi hiyo ya ligi.
1. Vurugu zilizofanywa na mashabiki wa Mbeya City kwenye dakika ya 66 kupelekea mchezo huo kusimama kwa dakika kadhaa wakati jeshi la Polisi likituliza vurugu hizo.
Wakati mchezo ukiendelea mashabiki wa Mbeya City walikuwa wakimrushia mawe mlinda lango wa Yanga Youthe Rostand ambaye mara kadhaa alilazimika kulikimbia lango kunusuru maisha yake.
Kwa kiasi kikubwa hali hiyo ilisababisha taharuki kwa wachezaji wa Yanga hivyo kuwaondoa mchezoni.
2. Tukio la Malima aliyetolewa nje kwa kadi nyekundu kurejea uwanjani kushangilia na wenzie baada ya Mbeya City kusawazisha bao kwenye dakika ya 90.
3. Kitendo cha Mbeya City kuzidisha idadi ya wachezaji waliostahili kuwepo uwanjani.
Kwenye dakika za nyongeza kuna mchezaji aliumia akatolewa nje kwa ajili ya kupatiwa huduma ya kwanza.
Wakati akiwa nje benchi la ufundi la Mbeya City lilimfanyia mabadiliko lakini baada ya kutibiwa akarudi tena uwanjani na kuendelea kucheza na hivyo kufanya idadi ya wachezaji wa Mbeya City kuwa 11 wakati tayari mchezaji mmoja alikuwa ametolewa nje kwa kdai nyekundu.

ADVERTISE HERE