August 11 2024 Yanga ilitwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Azam Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Zimepita takribani wiki saba Yanga imecheza mechi 9 pasipo kuruhusu bao
Ni sahihi kusema ukuta wa Yanga ndio bora zaidi kwa sasa katika soka la hapa Tanzania
Lakini pia Yanga imecheza zaidi ya miezi miwili pasipo kupoteza mchezo, iwe mechi za kirafiki au mashindano
Ilikuwa Julai 20 Yanga ilipoteza mechi wakati wa pre-season dhidi ya Augusburg inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani 'Bundesliga'
Benchi la ufundi la Yanga chini ya kocha Miguel Gamondi wamefanya kazi kubwa kuhakikisha timu inabaki katika ubora kwa muda mrefu
Maboresho yaliyofanyika katika dirisha lililopita yamemuongezea Gamondi wigo wa machaguo katika kikosi chake na kuifanya Yanga kuwa imara maradufu