Leo mchezo wa nusu fainali Ngao ya Jamii Wanawake kati ya Simba Queens dhidi ya Yanga Princess utapigwa saa 10 jioni katika uwanja wa KMC
Ni mchezo muhimu kwa Yanga Princess inayonolewa na kocha Edna Lema kupima utayari wa kikosi kwa ajili ya kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Wanawake msimu huu
Yanga Princess imefanyiwa maboresho makubwa katika dirisha lililopita la usajili hivyo Wananchi watarajie kuona timu tofauti kabisa na ile ya msimu uliopita
Ni mechi ngumu kwa Yanga Princess kwani inafahamika Simba Queens wamekuwa na timu imara kutokana na uwekezaji mkubwa wa muda mrefu waliofanya kwa timu yao
Mashabiki wa Yanga wameaswa kujitokeza kwa wingi KMC Complex kuipa hamasa Yanga Princess katika mchezo huo ambao hautakuwa na kiingilio
ADVERTISE HERE