Yanga ilishinda 1-0 mechi nane msimu uliopita

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Oct 2024
Yanga ilishinda 1-0 mechi nane msimu uliopita

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesisitiza katika kila mechi lengo ni ushindi ili kupata alama tatu, bila ya kujali idadi ya mabao yanayofungwa

Msimu huu presha imekuwa kubwa kwa Wananchi ikichagizwa na mijadala inayoendeshwa na wachambuzi katika vipindi vya michezo wakiponda ushindi wa bao 1-0 ambao Yanga wamepata katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Ken Gold na KMC

Gamondi ameshangazwa na mijadala hiyo ambayo inailenga zaidi ya Yanga licha ya ukweli katika ligi zipo mechi nyingi tu mshindi amefunga bao moja

"Jambo muhimu kwetu ni ushindi ili kupata alama tatu kwa sababu sio kila mechi tutafunga mabao mengi. Ukishinda bao 1 unapata alama tatu sawa sawa na ukishinda mabao mawili, matatu au zaidi"

"Yanga sio timu pekee iliyoshinda baadhi ya mechi kwa bao moja lakini mbona mjadala umeelekezwa kwetu tu?," alihoji Gamondi

Katika msimu uliopita kuna takribani mechi 11 Yanga iliibuka na ushindi wa tofauti ya bao moja

Mechi nane Yanga ilipata ushindi wa bao 1-0 wakati mechi tatu ilipata ushindi wa mabao 2-1

Lakini ikavunja rekodi kwa kutwaa ubingwa ikiwa na alama nyingi (80) katika mechi 30, kwa maana Wananchi walipoteza alama 10 msimu mzima

Msimu huu Yanga imeanza vyema kwa kushinda mechi zote tatu za mwanzo ikishinda 2-0 dhidi ya Kagera Sugar na 1-0 dhidi ya KMC na Ken Gold

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’