Gamondi akerwa na wanaobeza ushindi wa 1-0

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Sep 2024
Gamondi akerwa na wanaobeza ushindi wa 1-0

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesisitiza jambo muhimu kwa kikosi chake ni alama tatu kwani sio kila mechi watafunga idadi kubwa ya mabao

Yanga iliichapa KMC bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu uliopgwa uwanja wa Azam Complex, ukiwa ni ushindi wa pili mfululizo Yanga ikifunga bao bao moja

Akizungumza baada ya mchezo huo Gamondi aliwapongeza wachezaji wake kwa ari kubwa walioingia nayo katika mchezo huo lakini pia hakusita kuwapongeza wapinzani wake KMC kwani walikuwa madhubuti katika kujilinda

"Mimi nimefurahi kwa sababu tumeshinda, muhimu ilikuwa alama tatu. Wachezaji walicheza vizuri tulitengeneza nafasi nyingi kuliko wapinzani wetu"

"Nawapongeza KMC pia, walikuwa na nidhamu kubwa katika kujilinda, kipa wao amefanya kazi nzuri"

"Alama tatu ndio jambo muhimu kwetu, tungeweza kufunga mabao mawili au hata matatu lakini nafikiri kipa wa KMC alikuwa na siku nzuri sana leo (jana)"

"Kwangu mimi sio tatizo kushinda bao moja, inanishangaza Yanga inaposhinda bao moja mnasema lakini timu nyingine zikishinda moja mbona hamzungumzi?. Ni timu ngapi zimeshinda bao moja kwenye ligi msimu huu?", alihoji GamondiΒ 

Mchezo unaofuata kwa Yanga ni dhidi ya Pamba Jiji na utapigwa Alhamisi, Oktoba 03 katika uwanja wa Azam Complex

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’