Kipa wa Yanga, Djigui Diarra, ameingia anga za makipa bora Afrika baada ya kucheza mechi nne za hatua ya awali pasipo kuruhusu bao
Diarra amekuwa nguzo muhimu kwa Yanga, akisaidia Yanga kufika hatua ya makundi bila kuruhusu goli ndani ya dakika 360
Diarra ametumia dakika hizo katika mechi mbili za raundi ya kwanza dhidi ya Vital'O Burundi na Yanga ilishinda jumla ya mabao 10-0 ikianza kwa kushinda 4-0 na ziliporudiana ilishinda tena 6-0, kisha ikacheza mechi za raundi ya pili dhidi ya CBE SA ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 7-0.
Diarra aliendeleza umwamba kwa kuisaidia Yanga kushinda 1-0 ugenini jijini Addis Ababa, Ethiopia kisha wikiendi iliyopita ikicheza Uwanja wa Amaan Zanzibar, Yanga ilishinda tena 6-0 na kufanya kipa huyo na Yanga kwa jumla kucheza mechi nne bila ya kuokota mpira nyavuni
Aidha katika ligi kuu ya NBC, Diarra tayari ana 'cleansheet' mbili akikaa langoni pasipo kuruhusu bao katika mechi mbili dhidi ya Kagera Sugar na Ken Gold
Akiwa ameitumikia Yanga kwa misimu mitatu, Diarra bado yupo sana na Wananchi kwani mwezi Julai alisaini mkataba mwingine wa miaka mitatu ambao utamuweka Jangwani hadi mwaka 2027
Kwa hakika Yanga inajivunia mlinda lango huyo wa daraja la juu ambaye kwa sasa ndiye kipa namba moja wa timu ya Taifa ya Mali