Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amelalamikia kitendo cha klabu ya Mbeya City kufanya 'uhuni' kwa kuingiza mchezaji na kumuacha aendelee kucheza aliyepaswa kutoka baada ya kufanya mabadiliko.
Wakati mchezo ukiendelea Nsajigwa alimfuata Kamisaa wa mchezo huo na kumueleza kuwa Mbeya City ilikuwa na wachezaji 10 uwanjani.
Mbeya City ilipaswa kuwa na wachezaji tisa uwanjani baada ya Malima kutolewa nje kwa kuonyeshwa kadi mbili za njano.
Ni dhahiri mabadiliko yaliyofanywa na timu hiyo wakati mchezo ukielekea ukingoni, yalipelekea kuongeza idadi ya mchezaji mmoja huku aliyetakiwa kutoka akiendelea kucheza.
Mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 uligubikwa na vurugu za hapa na pale kutoka kwa mashabiki wa Mbeya City
Aidha, kitendo cha mashabiki kumrushia mawe mlinda lango wa Yanga Youthe Rostand hakikuwa cha kiungwana hata kidogo.
Kama mashabiki walikuwa hawaridhishwi na maamuzi ya refa, sasa ilikuwaje wakamrushia mawe mlinda lango wa Yanga?
Bila shaka hilo lilikuwa lengo la kumtoa mchezoni lililofanywa na mashabiki ambao waliamini alikuwa kikwazo kwa timu yao kusawazisha
Mwamuzi wa mchezo huo Shomari Lawi alikusanya mawe pamoja na vipande vya chupa alizorushiwa Rostand ikiwa ni sehemu ushahidi wa tukio hilo lisilokuwa la kiungwana.
Bila shaka Kamati ya Saa 72 itaichukulia hatua klabu ya Mbeya City kwa matukio hayo yaliyokuwa na lengo la kuvuruga mchezo.

ADVERTISE HERE