Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema ari na morali ya wachezaji kuelekea mchezo dhidi ya CBE SA iko juu na matumaini ni makubwa Yanga itaibuka na ushindi mnono katika mchezo huo
Yanga ilitua Zanzibar jana na usiku ikafanya mazoezi katika uwanja wa New Amaan Complex ambao mchezo wa mkondo wa pili kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya CBE SA utapigwa
"Leo (jana) timu imepata nafasi ya kufanya mazoezi ya kwanza katika uwanja wa New Amaan Complex. Nimeshuhudia ari na morali kubwa wachezaji wetu"
"Mimi niko na timu kwa muda mwingi. Mara nyingi wachezaji wakiwa katika hali hii basi tarajia ushindi wa mabao sio chini ya manne"
"Wachezaji wamepania kufyeka kichaka na kuipeleka Yanga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa kwa msimu wa pili mfululizo," alisema Kamwe
Vijana wa kocha Miguel Gamondi leo watakamilisha maandalizi yao tayari kwa mchezo huo utakaopigwa Jumamosi, saa 2:30 usiku









