Kikosi cha Yanga kimeondoka jijini Dar es salaam kuelekea Zanzibar tayari kwa mchezo wa mkondo wa pili kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya CBE SA ya Ethiopia
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Septemba 21 saa 2:30 usiku katika uwanja wa New Amaan Complex
Wakiwa mbele kwa bao 1-0 ushindi waliopata katika mchezo wa mkondo wa kwanza, Wananchi wanakwenda Zanzibar wakiwa na dhamira moja tu ya kumaliza kazi iliyobaki na kutinga hatua ya makundi










ADVERTISE HERE