Yanga Princess inayojiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya Wanawake 2024/25, leo ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mlandizi Queens katika dimba la KMC
Kinadada hao Wananchi wameibuka na ushindi wa mabao 5-1 ukiwa ni ushindi wa nne katika mechi za kirafiki walizocheza mpaka sasa
Kikosi cha Yanga Princess kinachonolewa kocha Edna Lema 'Mourinho' kinatoa matumaini kuwa msimu ujao wanakwenda kushindana ligi kuu ya Wanawake na sio kushiriki tu
Katika mechi za nyingine za kirafiki ambazo Yanga Princess wamecheza, waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mashujaa Queens, wakashinda mabao 16-0 dhidi ya Mtoni Queens na pia kuichapa Wisdom Queens mabao 8-0
Yanga Princess inajiandaa na mchezo wa nusu fainali Ngao ya Jamii dhidi ya Simba Queens utakaopigwa Septemba 24
