Mshambuliaji Prince Dube bado anastahili kuongoza safu ya ushambuliaji wa Yanga licha ya ukosoaji anaokumbana nao baada ya mechi za hivi karibuni
Juzi Dube aliifungia Yanga bao pekee la ushindi katika mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya CBA SA ya Ethiopia
Licha ya kukosa nafasi kadhaa kabla ya kufunga bao hilo, Dube aliendeleza wastani wake mzuri wa kufunga mabao tangu alipojiunga na Yanga msimu huu
Amepachika mabao manne katika mechi za mashindano, ambapo katika ligi ya mabingwa hatua hii ya awali amepachika mabao matatu mpaka sasa huku bao moja akifunga katika mchezo wa Ngao ya Jamii
Dube amepachika mabao sita katika mechi nane alizoitumikia Yanga mpaka sasa msimu huu. Huu ni uwiano mzuri wa mabao kwa mshambuliaji
Ni wazi kama atafanyia kazi changamoto ya kupoteza nafasi nyingine, pengine anaweza kuwa anaondoka na mpira katika kila mechi
Dube ametabiriwa kufanya makubwa akiwa na Yanga, takwimu zake zimeanza kuthibitisha kauli ya Rais wa Yanga Injinia Hersi Said kuwa kama mshambuliaji huyo atafunga chini ya mabao 20 msimu huu basi atakuwa amefeli