Wakati Yanga ikiwa nchini Ethiopia ambapo jioni ya leo watashuka uwanja wa Abebe Bikila kumenyana na CBE SA katika mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania kufuzu hatua ya makundi CAF CL, kule Pemba visiwani Zanzibar kutakuwa na shamrashamra za aina yake zilizoandaliwa na Wananchi
Saa tatu asubuhi kutakuwa supu, huu umekuwa utamaduni wa Yanga sasa, Wananchi wakiwa na jambo lao, lazima waanze na supu!
Jioni Wananchi watapata fursa ya kushuhudia mchezo dhidi ya CBE SA katika 'Big screen' kwenye uwanja wa Gombani, Pemba
Zoezi la uandikishaji wa Wanachama na mashabiki litakwenda sambamba na burudani hizi
ADVERTISE HERE