Hatutawadharau CBE SA - Mtine

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Sep 2024
Hatutawadharau CBE SA - Mtine

Mtendaji Mkuu wa Yanga Andre Mtine amesema timu iko salama Ethiopia na wako tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya CBE SA utakaopigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Abebe Bikila

Mtine ambaye ameongoza msafara wa Yanga huko Ethiopia, amesema hawatawadharau wapinzani wao kwa sababu anaamini hawakufika hatua hii ya mtoano kwa bahati mbaya

"Tumefika hapa salama na timu inaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo hapo kesho. Hali ya hewa hapa ni mvua inanyesha lakini tulifahamu mapema tutakutana na hali hii ya hewa"

"Tunakwenda kupambana uwanjani ili kupata matokeo mazuri hapa ugenini. Hatutawadharau wapinzani wetu kwani hakuna timu ndogo katika mashindano haya"

"Wao walishinda mechi za hatua iliyopita ndio maana wako hapa kama ilivyo upande wetu," alisema Mtine

Kikosi cha Yanga kilitua Ethiopia jana na kufanya mazoezi yao ya kwanza katika uwanja wa Abebe Bikila utakaotumika hapo kesho. Yanga itakamilisha mazoezi ya mwisho leo katika uwanja huohuo

Hali ya hewa sio mbaya sana, kuna mvua za hapa na pale ambapo jana timu ilifanya mazoezi katika mazingira ya mvua

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’