Leo Jumapili saa kumi kamili jioni Yanga itashuka kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya kuikabili Mbeya City katika moja ya michezo yake ya kiporo, ligi kuu ya Vodacom.
Mchezo huo ambao awali ulipangwa kupigwa May 01, 2018 umerudishwa nyuma kutokana na mkanganyiko wa ratiba inayoonyesha Yanga kutakiwa kucheza April 29 pia.
Tayari maandalizi ya mchezo huo yamekamilika. Kikosi cha Yanga kiliwasili mapema jana mkoani humo kwa usafiri wa Ndege na kufanya mazoezi mepesi jioni.
Yanga inahitaji kushinda mchezo huo ili kuweka hai matumaini yake ya kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo.
Katika mchezo wa mzunguuko wa kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Yanga iliifumua Mbeya City mabao 5-0

ADVERTISE HERE