Wachezaji wa Yanga ambao hawakuwa na majukumu ya timu za Taifa wameondoka nchini Alfajiri ya leo Alhamisi kuelekea Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza raundi ya pili ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya CBE SA
Nyota hao watawasili Addis Ababa na kuungana na wenzao ambao walikuwa katika majukumu ya timu za Taifa
Wachezaji ambao hawakujumuisha katika safari hiyo ni pamoja na kiungo Farid Mussa ambaye alifanyiwa upasuaji hivi karibuni akitarajiwa kuwa nje kwa miezi miwili
Beki Nickson Kibabage amepata msiba wa kufiwa na Baba yake Mzazi, amerejea nchini akitokea Ivory Coast alikokuwa na timu ya Taifa ya Tanzania
Tunatoa pole kwa familia ya Kibabage, Mwenye ez Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu
ADVERTISE HERE