Gamondi anaipigia hesabu kali CBE

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Sep 2024
Gamondi anaipigia hesabu kali CBE

Kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ametoa msimamo wake kwa kusema hataki kurudia makosa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, akipania kuinoa safu ya ushambuliaji kutumia kila nafasi watakazopata ili kufika mbali zaidi, huku akisisitiza kwamba hakuna aliyejihakikishia namba eneo hilo.

Gamondi alifunguka hayo baada ya kushuhudia timu ya taifa ya Tanzania β€˜Taifa Stars’ ikiambulia suluhu dhidi ya Ethiopia kwenye Uwanja wake Benjamin Mkapa juzi

Licha ya kikosi chake kuonekana kimekamilika, Gamondi amesema bado anahitaji kufanyia kazi baadhi ya maeneo hasa safu ya ushambuliaji ili kuhakikisha wanaongeza ufanisi katika kutumia nafasi nyingi wanazotengeneza

"Hatua hii ni muhimu na itategemea matokeo mazuri nyumbani na ugenini tunaanzia ugenini tunahitaji ushindi wa mabao mengi ili kukwepa kuondolewa kwa changamoto ya idadi ya mabao ya nyumbani na ugenini kama hatua ya robo fainali msimu uliopita"

"Kila mchezo ni muhimu kwetu tumeanza vizuri katika hatua ya awali kwa kushinda mechi zote mbili kwa idadi nzuri ya mabao. Natarajia hilo litaendelea hatua ijayo na kwenye hili sina mchezaji ambaye namtegemea eneo hilo, kila mchezaji wajibu wake ni kuipambania timu"

Gamondi alisema hana wasiwasi na ushindani atakaokutana nao kwani anauelewa ugumu wa michuano hiyo na wachezaji wake wanatambua umuhimu wa mchezo na malengo ya msimu huu.

"Tutaingia kwa kuwaheshimu wapinzani wetu tumeshasahau matokeo yaliyopita mipango ya mchezo ujao inaendelea vizuri na mipango ni kufanya vizuri ugenini ili kuja kumaliza mchezo kwenye uwanja wetu wa nyumbani,” alisema

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’