Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amewaalika mashabiki wa timu hiyo kujiunga katika Tawi la mtandaoni maalum kwa vijana, YANG Z
Tawi hilo litazinduliwa Jumamosi, Septemba 07 Upepo Beach Garden, Kawe jijini Dar es salaam
Aidha Kamwe amewataka Wanachama wote ambao tayari wamejisajili kufika katika uzinduzi huo ambapo watapatiwa kadi zao
"Jumamosi kuanzia saa 6 Kamili mchana tutafanya Uzinduzi wa Tawi jipya la Yang Z pale Upepo Beach Garden Kawe Dar es Salaam"
"Nawaomba Wanachama wote waliyojisajili kwenye Tawi hili tukutane na tuburudike kwa Pamoja"
"Naombeni tuzingatie mavazi yananyoendana na Beach, Na Wasanii ambao mnajua kuwa ni marafiki zetu tunawaomba mje kuwaburudisha Yang Z wote siku hiyo," alisema Kamwe
Tawi hilo tayari limesajili zaidi ya Wanachama 400