Aucho atastaafu soka akiwa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Sep 2024
Aucho atastaafu soka akiwa Yanga

Akiwa katika msimu wa nne tangu ajiunge na Yanga, kiungo Mganda Khalid Aucho ameweka wazi kuwa hafikirii kuondoka Yanga karibuni

Akihojiwa chombo kimoja cha habari nchini Uganda alikorejea kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa, Aucho alisema anajisikia furaha kuwa katika timu bora katika ukanda wa Afrika Mashariki

Aidha Aucho alibainisha kuwa mashabiki wa Yanga wana upendo mkubwa kwa wachezaji huku viongozi wa klabu wakihakikisha wanapata kila wanachostahili kwa wakati

"Nina furaha kucheza Yanga ndio maana nasema kwa sasa sifikii kuondoka kucheza sehemu nyingine labda itokee wenyewe waniambie basi imetosha"

"Hapa viongozi wanatujali sana wachezaji, kama ni mshahara tunalipwa kwa wakati, mashabiki wana upendo mkubwa kwa timu yao"

"Kiufupi mimi hapa nimefika, nitaendelea kupambana na kutoa mchango wake kwa timu hadi pale Rais wa klabu, Eng. Hersi, atakapoona imetosha," alisema Aucho

Tangu alipojiunga na Yanga mwaka 2021 akitokea klabu ya El Makas, Aucho amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Yanga akishinda mataji matatu ya ligi kuu, FA, Ngao mbili za Jamii huku akiwa sehemu ya kikosi kilichofanikiwa kutinga fainali ya CAF CC na robo fainali ya ligi ya mabingwa CAF CL

Mchezaji bora huyo wa mashabiki wa Yanga msimu uliopita, ni sahihi kusema ndiye injini ya Yanga katika eneo la kiungo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’