Yanga imemkabidhi rasmi Mwanamama Edna Lema mikoba ya kukinoa kikosi cha Yanga Princess
Baada ya misimu miwili isiyoridhisha, hatimaye Yanga Princess imerejeshwa mikononi mwa Lema ambaye alikaribia kuipa ubingwa wa ligi kuu ya Wanawake 2022/23
Jukumu la kwanza la Lema ni kukisuka upya kikosi cha Yanga Princess ambapo ni kama kazi imeanza upya baada ya kuachana na idadi kubwa ya wachezaji waliotumika msimu uliopita
Msimu uliopita Lema alikuwa Kocha Msaidizi wa Biashara United ya Mara ambapo yeye na wenzake katika benchi la ufundi walifanikiwa kuipa Biashara United nafasi ya kucheza play-off ya kupanda ligi kuu
Lema ana uzoefu mkubwa na soka la Wanawake ambapo alicheza kwa mafanikio kabla ya kuhamia katika majukumu ya ukufunzi
Karibu tena Lema...!