Wydad Athletic bado haijakata tamaa kumnasa mshambuliaji kinda Clement Mzize (20) ambaye katika kipindi cha wiki mbili amezungumzwa zaidi katika soka la Tanzania
Wydad wametuma ofa tatu kwa Yanga ambazo zote zilitolewa nje, Yanga wakiwataka matajiri hao kutoka Morocco kulipa takribani 2.7B kama ni lazima wamsajili Mzize sasa
Ukipita katika ukurasa wa Instagram wa Mzize utakutana na jumbe nyingi za mashabiki wa Wydad wakimshawishi nyota huyo aelekee Morocco
Ni kama kuna kampeni kubwa Wydad wanafanya nje ya uwanja kumshawishi Mzize 'aweke presha' kwa uongozi wa Yanga ili aondoke
Hata hivyo Mzize ameendelea kuheshimu mkataba wake na Yanga na kama ataondoka basi ni endapo Yanga itaridhia na sio vinginevyo
Mzize ana nafasi ya kun'gara katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu na pengine kuongeza thamani yake mara dufu
Wydad na hata Kaizer Chiefs ambazo zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili Mzize, hazishiriki mashindano ya CAF msimu huu