Shoo za Boka zinarejea leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Aug 2024
Shoo za Boka zinarejea leo

Mlinzi wa kushoto wa Yanga Chadrack Boka leo anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Wananchi kitakachoshuka dimbani mkoani Kagera kuikabili Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya NBC

Boka hakuonekana dimbani katika mechi mbili za hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Vital'o baada ya kuchelewa kupata vibali (ITC)

Yeye na mshambuliaji Jean Baleke walikosa mechi hizo lakini wanaweza kutumika kuanzia mechi ya hatua inayofuata ambapo Yanga itacheza na CBE ya Ethiopia kuwania tiketi ya kutinga makundi

Boka tayari amejizolea sifa kemkem kutoka kwa mashabiki wa Yanga kutokana na aina yake ya uchezaji

Kasi yake hasa anapopanda kushambulia ndio silaha yake kubwa, msimu huu huenda Yanga ikatengeneza mabao mengi kupitia upande wake

Baada ya 'kuwapima umri' walinzi wa Azam Fc katika mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii ambao Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 4-1, leo ni zamu ya Kagera Sugar

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
2h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’