Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kikosi chake kimejiandaa vyema kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa kesho Alhamisi katika uwaanja wa Kaitaba
Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Gamondi amesema wamejiandaa kwa kuzingatia aina ya mpinzani ambaye wanakutana nae
Gamondi amebainisha kuwa ana kumbukumbu ya mechi ya mwisho waliyocheza katika uwanja wa Kaitaba msmu uliopita ilimalizika kwa suluhu ya bila kufungana, hivyo ameitumia mechi hiyo kama funzo kuhakikisha wanapata ushindi hapo kesho
"Tumefika salama na tumejiandaa vya kutosha, tunakwenda kuanza msimu mpya tukiwa na hamasa kubwa. Sitaki kuangalia sana mchezo uliopita ingawa tulipata somo. Tumeshajiandaa kisaikolojia kucheza dhidi yao kwa kuzingatia namna yao ya uchezaji na mazingira ya uwanja"
"Huu ni mwanzo wa msimu, nimeshawaeleza wachezaji wangu nini mashabiki wanahitaji. Kiufupi wananchi wanahitaji alama tatu. Nafahamu mashabiki wetu wanatamani kweli tufunge magoli mengi, lakini kwetu sisi jambo la kwanza ni alama tatu," alisema Gamondi
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, beki Nickson Kibabage amesema wamejipanga kusahihisha makosa waliyofanya msimu uliopita na kupelekea wakakosa alama tatu katika uwanja wa Kaitaba
"Mchezo uliyooita katika uwanja huu hatukupata matokeo mazuri. Najua wachezaji wenzangu wanalitambua hilo. Bahati nzuri ni mchezo wa kwanza wa ligi tumeshajiandaa vyakutosha," alisema