Baada ya kusonga mbele raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kwa ushindi wa jumla wa mabao 10-0 dhidi ya Vital'o ya Burundi, Yanga itachuana na CBE ya Ethiopia katika hatua inayofuata
Mechi ya mkondo wa kwanza itapigwa Septemba 13 huko marudiano kupigwa Septemba 20 nchini Tanzania
Mshindi wa jumla katika mechi hizi atatinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amedokeza kuwa wanakusudia mchezo wao wa marudiano utakaopigwa hapa nyumbani watatumia Uwanja wa New Amaan Complex ili kuwapa fursa mashabiki wao waliopo Zanzibar.
"Malengo yetu ni kuendelea kuipeleka timu yetu karibu na wanachama na mashabiki wake kote nchini hivyo baada ya mechi hii ya awali kucheza hapa Dar es Salaam, kwa sasa raundi ya pili tunatarajia kuchezea kule visiwani Zanzibar," alisema Hersi
CBE ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchukua ubingwa wa kwao kwa mara ya kwanza tangu ianzishwe 1982.
Timu hiyo imeshiriki mara mbili michuano ya Afrika ambapo mara mbili ilicheza Kombe la Shirikisho Afrika na kutolewa katika hatua ya mtoano miaka ya 2005 na 2010, kisha msimu huu kuandika historia mpya kwa kushiriki Ligi ya Mabingwa.